Papert’s 8 Big Big Ideas of the Constructionist Learning Lab Translated in Swahili

Just want to share 8 Big Ideas of the Constructionist Learning Lab in Swahili. At least, Est Africa Community and other Swahili speakers can learn more about the concepts of constructionism.

Mnamo mwaka 1999, Seymour Papert, baba wa elimu ya kiteknolojia, alianzisha utafiti katika mradi wake alipotengeneza maabara ya ujenzi uliojaa teknolojia, kimradi zaidi, ya-kikarne ndani ya gereza inayoitwa Maine walipokua wamefungiwa vijana wenye matatizo. Habari ya maabara ya ujenzi imeandikwa kwenye ripoti ya Gary Stager, “An Investigation of Constructionism in the Maine Youth Center.” (Utafiti wa ujenzi ndani ya kituo cha vijana cha Maine). Ripoti hii iliandikwa katika chuo cha Melbourne mwaka 2006. Gary alichangia mada katika kitabu chetu kinachoitwa, Invent To Learn: Making, Thinkering, and Engineering in the Classroom, punde tuu baada ya kuanzishwa kwa mradi wa miaka mitatu, Papert aliandika Mawazo manane yalisababisha kuanzishwa kwa maabara ya kujifunzia ujenzi (constructist learning lab). Japokua haichoshi, orodha hii inarahisisha kuelewesha ujenzi (constructionism) kwa watu wote.”

Mawazo 8 yaliyo sababisha kuanzishwa kwa Constructionist Learning Lab.
Imeandikwa na Dr. Seymour Papert

Wazo la kwanza ni kujifunza kwa kutenda. Sisi wote huwa tunajifunza vizuri wakati kujifunza ni sehemu ya kufanya kitu kinacho tuvutia. Twajifunza vizuri Zaidi tunapo tumia kile tulicho jifunza ili tufanye kile tunachokitaka

Wazo la pili ni teknolojia kama vifaa vya kujenga. Kama unaweza kutumia teknolojia ili kutengeneza vitu, unaweza ukatengeneza vitu vingi na vyenye mvuto. Pia unaweza kujifunza mengi zaidi unapotengeneza hivo vitu. Hii ni kweli Zaidi inapofikia kwenye teknolojia ya kidigitali: kompyuta za aina zote ikiwemo Lego inayodhibitiwa kwa kompyuta ndani ya maabara yetu.

Wazo la tatu ni raha itokanayo na ugumu. Huwa tunajifunza vizuri na kufanya kazi vizuri pale ambapo tunafurahiya yale tunayoyafanya. Kuyafurahia haimaanishi kwamba ni rahisi. Raha nzuri Zaidi ni raha ya ugumu wa jambo. Mashujaa katika michezo wanafanya kazi kwa bidii ili wafanye vizuri katika michezo. Seremala anayefanikiwa Zaidi hufurahia useremala. Mfanya biashara mzuri hufurahia kuunda mitandao ya kibiashara.

Wazo la nne ni kujifunza jinsi ya kujifunza. Wanafunzi wengi hudhani kwamba njia pekee ya kujifunza ni kufundishwa. Hii ndio sababu moja inayowafanya kutofaulu katika masomo na katika Maisha. Kitu kimoja ambacho unahitaji kufahamu ni kuwa hamna mtu ambaye anaweza kukundisha kila kitu. Unahitaji kuchukuwa wajibu wa masomo yako mwenyewe.

Wazo la tano ni kuchukuwa muda-muda unawofaa ajili ya kazi. Wanafunzi wengi wakiwa shuleni wanazowea kuambiwa: fanya hiki, fanya kile kila saa. Ikiwa hamna mtu wa kuwaambia cha kufanya, huwa wanaboreka. Maisha sivyo yalivyo. Ili ufanye kitu cha muhimu, unahitaji kujifunza kutumia muda wako vizuri. Hili ndilo funzo gumu la idadi kubwa ya wanafunzi wetu.

Wazo la sita ndilo muhimu kuliko yote: huwezi kupatia bila kukosea. Hamna kitu muhimu kinachowezekana kwa mara ya kwanza. Njia pekee ya kupatia ni kuangalia kwa makini kilicho tokea wakati ulipokosea. Ili ufanikiwe unahitaji kuwa huru kukosea njiani.

Wazo la saba ni tujifanyie sisi tunayowafanyia wanafunzi wetu. Tunajifunza kila siku. Tuna uzowefu wakutosha kwa miradi mingi inayotaka kufanana ila kila mmoja una upekee wake. Hatuna wazo Fulani la jinsi mambo yatakavyokwenda. Tunafurahia tunayoyafanya ila tunategemea kuwa yatakuwa magumu. Pia tunategemea kutumia muda wa kutosha kuelewa wazo hili. Kila changamoto tunayokutana nayo tunaichukulia kama na fasi ya kujifunza. Fundisho kuu tunaloweza kuwapa wanafunzi wetu ni kutuona tukiangaika ili tujifunze

Wazo la nane ni kuwa tunaingia sasa ulimwengu wa kidigitali ambapo kufahamu teknolojia ya kidigitali ni muhimu kama ilivo kusoma na kuandika. Kwa hiyo kujifunza mambo ya kompyuta ni muhimu kwa siku zijazo za wanafunzi wetu ila sababu muhimu Zaidi ni kuzitumia sasa katika masomo yao.

 

Rudishwa Kutoka Kiingereza na Kiswahili kwa Kuzingatia:
In Stager, G. An Investigation of Constructionism in the Maine Youth Center. Doctoral dissertation. The University of Melbourne. 2006.

4 Comments

Comments are closed.